• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Mchezo wa Ligi ya Europa watibuka baada ya droni yenye bendera kuruka uwanjani

  (GMT+08:00) 2019-10-04 09:44:02

  Mchezo wa Ligi ya Europa kati ya F91 Dudelange na FK Qarabag ulisitishwa kwa muda baada ya droni kuonekana kuruka kwenye uwanja. Mchezo huo ulisimama kwa dakika 15 kufuatia kuonekana kwa droni iliyobeba bendera. Wachezaji wa Dudelange na Qarabag, za Azerbaijan, walijaribu kuishusha chini droni hiyo kwa kuipiga kwa mpira. Tukio hilo lilitokea katika kipindi cha kwanza cha mtanange ulioshuhudia Qarabag wakishinda 4-1. Mlinda mlando wa Bosnia-Herzegovina Asmir Begovic, ambaye yupo kwa mkopo kwenye klabu ya Bournemouth iliyopo kwenye Premier League ya Uingereza hadi Januari alikuwa akilinda lango la Qarabag.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako