• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" latoa fursa mpya kwa maendeleo ya pamoja ya dunia

    (GMT+08:00) 2019-10-05 17:17:35

    Katika maadhimisho ya miaka ya 70 ya Jamhuri ya Watu wa China, rais Xi Jinping wa China ametoa hatuba mara nyingi akisisitiza kuwa wananchi wa China wanapaswa kushirikiana na watu wa nchi mbalimbali duniani katika kuhimiza jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, ambayo inatiliwa mkazo mpya na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" alilotoa mwaka 2013.

    Katika miaka hiyo sita pedekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limelipatia ongezeko la uchumi wa dunia nguvu mpya, kuleta busara za China katika kutatua suala la kukosekana kwa uwiano kwenye maendeleo ya dunia, na limekuwa njia muhimu ya kuboresha utatuzi wa migogoro duniani. Ripoti ya uchunguzi kutoka Benki ya Dunia imeonyesha kuwa pendekezo hilo litawasaidia watu milioni 7.6 kutoka nchi husika waondokane na umaskini mkali, wengine milioni 32 waondokane na umaskini wa katikati, kuifanya biashara ya nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo hilo iongezeke kwa asilimia 2.8 hadi 9.7, kuifanya biashara ya dunia iongezeke kwa asilimia 1.7 hadi 6.2, kuyafanya mapato ya dunia yaongezeke kwa asilimia 0.7 hadi 2.9.

    Hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu, nchi 136 na mashirika 30 ya kimataifa yamesaini nyaraka za ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na China. Wazo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja limetajwa mara nyingi kwenye azimio la Umoja wa Mataifa, likiambatana na wazo la amani na usalama la Umoja wa Mataifa, na kulingana na maslahi ya pamoja ya nchi mbalimbali duniani.

    Hali halisi ya miaka hiyo sita imeonyesha kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" si "mtego wa deni", bali ni zawadi ya kuwanufaisha watu, na si nyezo ya siasa za kijiografia, bali ni fursa ya maendeleo ya pamoja. Hiyo ndiyo sababu kuu pendekezo hilo la China linakaribishwa na kuridhiwa na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako