• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Korea Kaskazini wapongezana miaka 70 ya uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2019-10-06 17:41:44

    Rais Xi Jinping wa China na kiongozi Kim Jong-un wa Korea Kaskazini wamepeana pongezi kwa nchi zao kutimiza miaka 70 tangu zianzishe uhusiano wa kibalozi.

    Rais Xi Jinping amesema kuwa matunda mengi ya mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili yamehimiza maendeleo ya mambo ya ujamaa na kubeba jukumu muhimu katika kulinda amani na utulivu wa kikanda.

    Naye Kiongozi Kim Jong-un amesema kuwa ana nia ya kufanya juhudi pamoja na Rais Xi Jinping katika kuimarisha na kuendeleza urafiki wa China na Korea Kaskazini, kulinda mambo ya ujamaa kwa urafiki na mshikamano, na kulinda amani na utulivu wa Penisula ya Korea na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako