• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachina watalii katika sikukuu ya siku ya taifa

    (GMT+08:00) 2019-10-07 08:46:41

    Mapumziko ya siku ya taifa huwa msimu wa utalii nchini China. Takwimu zilitolewa leo zinaonesha kuwa, katika siku nne za kwanza za mapumziko za sikukuu hiyo, idadi ya Wachina waliotalii ndani ya nchi ilifikia bilioni 542, ambalo ni ongezeko la asilimia zaidi ya nane ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, na pato la utalii lilizidi dola za kimarekani bilioni 63.75, na kuongezeka kwa asilimia 8.58.

    Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, Ili kuwawezesha watalii watazame maadhimisho ya miongo saba tangu kuasisiwa kwa China mpya, skrini kubwa za LED zimewekwa katika maeneo ya kitalii, mitaa ya kihistoria na mahali pengine penye umati wa watu. Kwenye uwanja wa mtaa wa Oufenghuajie mjini Yancheng mkoani Jiangsu, wakazi na watalii waliweza kutazama moja kwa moja maadhimisho makubwa yaliyofanywa kwenye uwanja wa Tian'anmen mjini Beijing. Bibi Wang Yanmin anasema,

    "Rais Xi Jinping amesema mustakabali wa China utakuwa mzuri zaidi. naamini kuwa chini ya uongozi thabiti wa Chama cha Kikomunisti cha China, taifa letu litakuwa na ustawi zaidi."

    Magari 70 yaliyopambwa kwa maua kwa ajili ya maadhimisho yaliyofanywa kwenye uwanja wa Tian'anmen yanaoneshwa sehemu mbalimbali mjini Beijing, na kuwavutia watalii wengi.

    "Nimefurahi sana baada ya kuona gari hilo, kwani limeonesha maendeleo na ustawi wa taifa letu."

    "Nchi yetu inaendelea kwa kasi, ninaona ustawi wa taifa letu."

    Miji yenye mabaki ya makumbusho ya mapinduzi ikiwemo Beijing, Jinggangshan, Zunyi, Nanchang na Yanan imewavutia watalii wengi. Bw. Tang pamoja na mtoto wake walitembelea Jumba la Makumbusho la Mapigano ya Xiangjiang lililoko mjini Quanzhou mkoani Guangxi. Anasema,

    "Nimemleta mtoto wangu hapa ili kumfahamisha kuwa maisha yenye amani ya hivi leo hayakupatikana kwa urahisi."

    Bibi Xu kutoka mkoa wa Jiangsu alikwenda mkoa wa Shanxi kwa gari, ili kutembelea Jumba la Makumbusho la Mapigano ya Pingxingguan dhidi ya wavamizi wa Japan. Anasema,

    "Nimeendesha gari kwa zaidi ya saa nane, ili kutoa heshima kwa mashujaa wetu waliojitoa mhanga kwa ajili yetu. Nataka kuwa na mapumziko yenye maana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako