• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MASUMBWI: Bondia wa Tanzania, Alphonce Mchumiatumbo agaragazwa chini n Mrusi Arstan Yellev kwa (TKO)

  (GMT+08:00) 2019-10-07 10:25:21

  Bondia namba moja wa uzito wa juu Tanzania, Alphonce Mchumiatumbo amepigwa na Mrusi, Arstan Yellev kwa Technical Knock Out (TKO) nchini Urusi usiku wa kuamkia jana Jumapili Oktoba 6, 2019. Katika mpambano huo wa raundi 8, Mchumiatumbo alipigwa TKO kwenye raundi ya kwanza, Ambapo bondia Arslan Yallyev alimsokomezea masumbwi mawili mazito yaliyomwangusha chini Mchumitumbo mara mbili na kujikuta akisalimu amri. Kocha Mtanzania aliyeambatana na bondia huyo, Anthony Rutha amesema refa alilazimika kumaliza pambano baada ya Mtanzania huyo kupelekwa chini mara mbili mfululizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako