• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Southampton yarambishwa mchanga na Chelsea, nao Manchester City mambo yaenda mrama kwa Wolves

  (GMT+08:00) 2019-10-07 10:26:30

  Tammy Abraham na Mason Mount wa Chelsea wameonesha furaha yao ya kuitwa timu ya taifa ya Uingereza kwa kuitoa makamasi Southampton iliyokuwa ikitapa jana kwa 4-1. Abraham, Mount na mchezaji mwenzao wa Blues Fikayo Tomori wote wametajwa na Meneja wa Uingereza Gareth Southgate katika kikosi cha michuano ijayo ya kufuzu mashindano ya Euro 2020 huko Jamhuri ya Czech na Bulgaria. Abraham ana magoli tisa kwenye mashindano yote aliyoichezea Chelsea katika msimu huu. Nao Manchester City mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi Kuu England inayonolewa na Pep Guardiola mambo yao yameanza kuwa magumu baada ya jana kupoteza mchezo wake wa pili kwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Wolves. City ikiwa uwanja wa nyumbani, Etihad ilikubali kuona nyavu zake zikitikiswa dakika ya 80 na 90 huku mfungaji akiwa ni Adama Traore. Ushindi huo unaifanya City kubaki nafasi ya pili baada ya kucheza michezo minane ikiwa na pointi zake 16 na imefunga mabao 18.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako