Na kufikia sasa kuna vibanda au vitu 28 vya biashara katika maeneo yenye utajiri wa madini.
Vituo vya kuuza na kununua vya serikali ni miradi ya Rais John Magufuli ya kuboresha biashara ya madini kufaidi sio tu mashirika ya kimataifa lakini pia wachimbaji wadogo, madalali, na wafanyabiashara.
Kujengwa kwa vituo hivyo ni njia moja ya kuboresha na kutoa uwazi mkubwa katika sekta ya madini ya nchi, na kuzuia ujumuishaji wa madini na ukwepaji kodi.
Mnamo 2018/19,mchango wa madini kwa Pato la Taifa umeongezeka kwa asilimia tano, kutoka asilimia 4.8 mwaka uliopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |