• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Pogba ataka Manchester United wamlipe £600,000 kwa wiki

  (GMT+08:00) 2019-10-08 08:58:42

  Mino Raiola ambaye ni wakala wa kiungo Paul Pogba amedokeza kuhusu uwezekano wa nyota huyo mzawa wa Ufaransa kubanduka uwanjani Old Trafford mwanzoni mwa Januari 2020 iwapo Manchester United watashindwa kumlipa kiasi cha £600,000 kwa wiki. Pogba ambaye amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Man-United, hakuwa sehemu ya kikosi cha waajiri wake kilichochuana na Newcastle United katika kipute cha EPL Jumapili uwanjani St James Park. Kwa upande wao, Man-United wamesisitiza kwamba hawana pupa yoyote ya kuongeza mkataba wa Pogba ambaye alikuwa sehemu muhimu zaidi katika kampeni za Ufaransa waliotawazwa mabingwa wa fainali za Kombe la Dunia zilizoandaliwa Urusi mwaka 2018. Iwapo Man-United watampatia Pogba mkataba mpya kwa malipo ya hadi £600,000 kwa wiki kama anavyodai wakala wake, basi atakuwa amekifikia kiwango cha nyota Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Juventus.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako