• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • BAISKELI: Timu Rwanda yafanya vibaya mbio za baisklei za Tour de Vendée

  (GMT+08:00) 2019-10-08 08:59:49

  Timu ya taifa ya waendesha baiskeli ya Rwanda imemaliza vibaya mbio za Tour de Vendée zilizofanyika Ufaransa baada ya mwendesha baiskeli mmoja tu kati ya sita kumaliza mbio hizo. Ukiachilia mbali Jean-Claude Uwizeye aliyemaliza katika nafasi ya 65, waendesha baiskeli wengine wa timu Rwanda walikuwa miongoni mwa waendesha baiskeli 33 walioshindwa kumaliza mpambano huo wa km 200. Uwizeye, mwenye miaka 25, alivuka mstari wa kumalizia dakika 6 na sekunde 3 nyuma ya bingwa Mfaransa Marc Sarreau. Mwendesha baiskeli huyo wa Rwanda alishinda Tour de Guyane mwezi Agosti. Katika kikosi cha waendesha baiskeli 17, ambacho kinajumuisha timu mbili za World Tour, Rwanda ilikuwa timu pekee ya taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako