• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KASHFA: Aliyekuwa Rais wa TFF, Michael Wambura aachiwa huru na mahakama, atakiwa kulipa zaidi Sh Milioni 100

  (GMT+08:00) 2019-10-08 09:00:19

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam jana ilimuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura kwa sharti la kulipa kiasi cha zaidi ya Shilingi milioni mia moja laki tisa kwa awamu tano. Na hiyo ilifuatia upande wa mashitaka kumfutia Wambura mashitaka ya uhujumu uchumi yenye mashitaka 17 yakiwemo ya kutakatisha zaidi ya Sh. Milioni 100 na kumsomea mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kosa ambalo alikiri kutenda. Katika mashtaka hayo 17; shtaka moja ni la kughushi, shtaka moja la kutoa na kuwasilisha nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha haramu katika kesi ya uhujumu uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako