• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SHANGHAI MASTERS: Andy Murray amshinda Muargentina Juan Ignacio Londero

  (GMT+08:00) 2019-10-08 09:02:21

  Muingereza Andy Murray ameendeleza kichapo chake katika mashindano ya mtu mmoja mmoja baada ya kumtambia Muargentina Juan Ignacio Londero katika raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Shanghai. Murray, alianza vibaya katika seti ya ufunguzi hata hivyo alijikaza kiume na kushinda seti 2-6 6-2 6-3. Murray Amefanikiwa kufikia hatua ya robo fainali ya mchezaji mmoja mmoja katika muda wa zaidi ya mwaka mmoja kwenye mashindano ya wazi ya China mapema mwezi Oktoba. Murray, ambaye ameshinda taji la Shanghai katika mashindano matatu – mwaka 2010, 2011 na 2016 alijiongeza baada ya kutolewa kijasho mara mbili na mchezaji huyo namba 56 duniani. Mshindi huyo wa Grand Slam mara tatu ambaye sasa yupo nafasi ya 28 duniani, ataingia kwenye mechi ya raundi ya pili dhidi ya Muitalia Fabio Fognini aliye nafasi ya 12 duniani, ambaye alishinda katika raundi ya kwanza dhidi ya Mmarekani Sam Querrey.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako