• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ngezeko la chai kimataifa lapunguza bei Kenya

  (GMT+08:00) 2019-10-08 18:58:07

  Mapato ya chai kwa wakulima wadogo wadogo nchini Kenya yamepungua kwa asilimia 18 kufuatia ongezeko la bidhaa hiyo kwenye soko la kimataifa.

  Mkurungezi wa shirika la chai nchini humo KTDA Lerionka Tiampati amesema hali hiyo imesababisha kupungua kwa mapato katika viwanda vya chai.

  Katika kipindi cha mwaka mmoja uzalishaji wa chai duniani ulifikia kilioni bilioni 5.8 huku mahitaji yakiwa ni kilo bilioni 5.6.

  KTDA imesema mapato ya chai katika mwaka uliokamilika mwezi Juni yalifikia dola bilioni 7.1 ikilinganishwa na dola bilioni 8.8 za mwaka uliotangulia.

  Kufuatia kuongezeka kwa chai sokoni sasa wakenya watapokea dola 41 kwa kilo moja ya majani chai ghafi lakini bei ya awali ilikuwa ni dola 52.8.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako