• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baba wa taifa la Zambia asema China ni rafiki mwaminifu wa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-10-09 09:37:27

    Baba wa Taifa la Zambia Bw. Kenneth Kaunda ni rafiki mkubwa wa China. China yake Zambia ilipata uhuru tarehe 24 Oktoba mwaka 1964 kutokana na juhudi zake na wananchi wenzake, na siku moja baadaye ilianzisha uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China. Bw. Kaunda kwa muda mrefu amehimiza maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya nchi yake na China na kati ya Afrika na China.

    Bw. Kenneth Kaunda alitembelea China mara nyingi, na kuwa na urafiki mkubwa wa viongozi mbalimbali wa China. Mwaka 1967 katika ziara yake ya kwanza nchini China, Bw. Kaunda na viongozi wa China waliamua kujenga Reli ya TAZARA inayounganisha Zambia na Tanzania. Bw. Kaunda mwenye umri wa miaka 95 anaona reli hiyo inaonesha urafiki wa kweli kati ya China na Afrika. Anasema,

    "Wakati huo serikali za nchi nyingine na mashirika ya kimataifa yote yalikataa kutusaidia kujenga reli hiyo. Lakini China ilitoa msaada wa watu na mali ili kujenga reli hiyo yenye urefu wa kilomita 1,860. Reli ya TAZARA inajulikana kama 'Reli ya Uhuru', na ilitupatia njia ya kufika baharini."

    Bw. Kaunda anaiunga mkono kithabiti China, na alifanya kazi muhimu kuisaidia China kurudi kwenye Umoja wa Mataifa, na yeye ni mmoja wa marafiki wakubwa wa Afrika "walioibeba China kuingia kwenye Umoja wa Mataifa". Mara kwa mara Bw. Kaunda alisema Zambia na China ni marafiki wa kudumu, na kupongeza ushirikiano wa dhati uliopo kati ya nchi hizo. Anaona China inazitendea nchi za Afrika kwa usawa na kuheshimiana, na kutafuta maendeleo ya pamoja. Anasema,

    "Kutokana na uzoefu wangu wa kuongoza mapinduzi na utawala wa Zambia, nimetambua kuwa China ambayo ni nchi yenye ushawishi mkubwa inapenda kutendeana kwa usawa na nchi ndogo, na kufanya ushirikiano nazo kwa udhati. Tunapaswa kutumia fursa ya kushirikiana na China kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii barani Afrika."

    Bw. Kaunda amezitaka nchi mbalimbali za Afrika kuhimiza ushirikiano wa kirafiki na China, na kuongeza uwezo wa kujiendeleza, akisema,

    "China inazisaidia nchi za Afrika ikiwemo Zambia kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii. Lakini hadi sasa nchi za Afrika hazijatumia vya kutosha fursa inayoletwa na China. Nchi hizo zinapaswa kuchukua hatua za pamoja ili kubadilisha sura ya bara la Afrika, na kupunguza umaskini. Ikilinganishwa na nchi nyingine duniani, tumebaki nyuma kimaendeleo. Hivyo tunatakiwa kuharakisha hatua ya kushirikiana na China, ili kutimiza malengo ya maendeleo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako