• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AC Milan yamtimua kazini kocha wao mkuu Marco Giampaolo

  (GMT+08:00) 2019-10-09 10:32:45

  Klabu ya AC Milan ya Italia usiku wa October 8, 2019 imefikia maamuzi mazito ya kumfukuza kazi kocha wao mkuu Marco Giampaolo baada ya kuifundisha timu hiyo katika michezo saba pekee. AC Milan wamefikia maamuzi hayo ya kumtimua kazini Giampaolo baada ya klabu yao kuendelea kuwa katika hali mbaya Serie A na kuwa katika mwenendo usioridhisha toka kocha huyo alipomrithi Gennaro Gattuso mwezi Juni. Katika mechi 7 Marco Giampaolo alizoziongoza chini ya AC Milan katika Serie A ameshinda michezo mitatu na kupoteza minne huku timu ikiwa nafasi ya 13 kwa kuwa na point 9 lakini ni point 3 dhidi ya timu zilizopo katika nafasi za kushuka daraja. Koch wa zamani wa Fiorentina na Inter Milan Stefano Pioli anaripotiwa kuziba pengo Giampaolo na kuifunda AC Milan ambao ni mabingwa mara saba wa Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako