• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Chama cha Riadha Uingereza aachia ngazi kufuatia kashfa ya Salazar

    (GMT+08:00) 2019-10-09 10:33:04

    Chama cha Riadha cha Uingereza kimetangaza kuwa Mkurugenzi wake Mkuu wa Riadha Neil Black anaachia ngazi nafasi yake, baada ya kusema ataitathmini nafasi yake kufuatia Alberto Salazar ambaye ni kocha wa zamani wa bingwa wa Olimpiki Mo Farah kufungiwa kwa miaka minne kushiriki riadha kwa makosa ya kutumia dawa za kusisimua misuli. Adhabu hiyo imekuja baada Shirika la Kupambana na Dawa za Kusimumua Misuli la Marekani (Usada) kuchunguza shughuli za mradi wake wa mafunzo wa Oregon huko Potland unaodhaminiwa na Nike. Black alikuwa ndio mkuu wakati Chama cha Riadha cha Uingereza kilipomteua Salazar kama mshauri kwenye mradi huo mwaka 2013. Mwaka 2015, wakati Usada ilipoanza kuchunguza juu ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli Salazar alikuwa akimfunza Farah, ambaye alimsaidia kuwa bingwa mara nne wa Olimpiki katika mbio ndefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako