• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mchenga Bball Stars mabingwa wa Sprite Bball Kings 2019

  (GMT+08:00) 2019-10-09 10:33:20

  Michuano ya Sprite Bball Kings imemalizika jana kwa Mchenga Bball Stars kuibuka mabingwa. Mchenga imeshinda ubingwa baada ya kufanikiwa kushinda michezo mitatu ya fainali dhidi ya Tamaduni, ambapo katika mchezo wa tatu wa jana uliofanyika katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay, Mchenga imeshinda kwa vikapu 115 dhidi ya 109 vya Tamaduni, huku Baraka Sadick akifunga pointi 52, rebounds 3 na assists 3. Ubingwa huo ni wa tatu mfululizo kwa Mchenga Bball Stars tangu mashindano yalipoanzishwa mwaka 2017, na mchezaji Baraka Sadick ameshinda tuzo ya MVP wa mashindano kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kushinda msimu uliopita akiwa na timu hiyo. Bingwa wa michuano Mchenga Bball Stars imejinyakulia kitita cha Shilingi milioni 10 za Kitanzania, mshindi wa pili Tamaduni akijinyakulia kitita cha Shilingi milioni 3 huku Baraka Sadick aliyepata tuzo ya MVP akijishindia Shilingi milioni 2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako