• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tammy Abraham asema Uingereza itaondoka uwanjani kama wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi

  (GMT+08:00) 2019-10-09 10:33:55

  Tammy Abraham amesema Uingereza imejiandaa kuondoka uwanjani kama wanalengwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi kwenye mchezo wao wiki hii wa kufuzu kucheza Kombe la Ulaya mwaka 2020. Uingereza itavaana na Jamhuri ya Czech Ijumaa halafu itacheza na Bulgaria siku ya Jumatatu kwenye uwanja uliofungwa baadhi ya sehemu kwasababu ya tabia za kibaguzi walizoonesha mashabiki mwezi Juni. Abraham amesisitiza kuwa kama ikimtokea mmoja wao ni sawa na kuwatokea wote. Naye Harry Kane amesema kama hawana furaha, au kama mchezaji hana furaha, basi wote watatoka kiwanjani kwa pamoja. Uefa imeamuru kufungwa kwa sehemu ya uwanja wa taifa wa Bulgaria kufuatia vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyofanywa na mashabiki wao kwenye michezo ya kufuzu kombe la Ulaya mwaka 2020 dhidi ya Jamhuri ya Czech na Kosovo mwezi Juni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako