Waziri ambaye pia ni msaidizi maalum wa waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Arkebe Oqubay amezitaka nchi za Afrika kuendeleza mikakati yao wenyewe ya jinsi ya kufaidika na fursa nyingi zinazotokana na uhusiano na China.
Akizungumza katika ufunguzi wa semina kuhusu mkakati wa mageuzi ya kiviwanda iliyofanyika mjini Accra, Ghana, Oqubay amesema China ni mfano wa kuigwa katika maeneo mbalimbali kama vile kilimo cha kisasa, na Afrika inapaswa kuiga ujuzi wa China ili kuendelea zaidi.
Amesema sera bora, zikiandamana na uongozi imara vinatakiwa ili kutimiza mageuzi hayo na maendeleo yanayotafutwa na wananchi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |