• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mawaziri wakuu wa Pakistan na Visiwa vya Solomon

    (GMT+08:00) 2019-10-09 18:56:18

    Rais Xi Jinping wa China leo kwa nyakati tofauti amekutana na waziri mkuu wa Pakistan Bw. Imran Ahmed Khan Niazi, na waziri mkuu wa Visiwa vya Solomon Bw. Manasseh Sogavare mjini Beijing.

    Rais Xi amesema China na Pakistan ni wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa siku zote, na itaiunga mkono kithabiti Pakistan juu ya maslahi makuu na ufuatiliaji mkuu. Amesema pande zote mbili zinapaswa kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu na ya kimkakati, na kwamba China inatilia mkazo hali ya Kashmir, na kuiunga mkono Pakistan kulinda haki yake halali. Amesema China inataka pande husika kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo.

    Kwa upande wake, Bw. Imran Khan amesema Pakistan inaishukuru China siku zote inashikilia kanuni zinazohusika na kulinda haki halali, na inataka kuimarisha mawasiliano, uratibu na ushirikiano na China.

    Akizungumza na waziri mkuu wa Visiwa vya Solomon Bw. Manasseh Sogavare, rais Xi amesema katika siku za karibuni China na Visiwa vya Solomon zimeanzisha rasmi uhusiano wa kibalozi chini ya msingi wa kanuni ya kuwepo kwa China Moja, jambo linaloendana na wakati na kuwanufaisha wananchi wa nchi hizo mbili. Amesema China inapenda kushirikiana na Visiwa vya Solomon kuimarisha mawasiliano na ushirikiano ndani ya mfumo wa pande nyingi, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea.

    Naye Bw. Manasseh Sogavare amesema, Visiwa vya Solomon vinapenda kushirikiana na China kwenye sekta mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, kilimo, uvuvi, na utalii, ambao ni mfano mzuri wa kuigwa katika Ushirikiano wa Kusini na Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako