• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vijana 10,000 washiriki Mkutano wa Youth Connekt mjini Kigali,Rwanda

  (GMT+08:00) 2019-10-09 19:07:46
  Mkutano wa Vijana wa Youth Connekt ulianza leo jijini Kigali katika jumba la mikutano la Kigali Arena.

  Mkutano huo umewaleta pamoja vijana 10,000 kutoka sehemu mbalimbali Afrika.

  Kaulimbiu ya mkutano huo ni : "Kuipiga jeki Afrika ndogo yenye bidii".

  Ufunguzi rasmi wa mkutano huo ulishirikisha wazungumzaji ikiwa ni pamoja wajasiriamali watajika,wanariadha wa kimataifa na washauri wa vijana.

  Miuongoni wa waliozungumza ni pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji wa Mara Group,Asish Takkar.

  Mara Group ni kampuni ya kwanza kutengeneza simu za kileo au simu janja kote barani Afrika.

  Kiwanda ambacho kinapatikana katika eneo la kiuchumi la Kigali,kilifunguliwa jumatatu na Rais Paul Kagame na kitakuwa na uwezo wa kutengeneza simu milioni 1 kwa mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako