• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wahudumu wa Matatu (daladala) watishia kufanya mgomo

  (GMT+08:00) 2019-10-09 19:08:47
  Wamiliki wa magari ya usafiri wa umma maarufu "matatu" kutoka ukanda wa mlima Kenya wametishia kusitisha biashara ili kupinga agizo la serikali linalowataka kufunga vidhibiti mwendo vipya katika magari yao.

  Wahudumu hao wa matatu wanaitaka Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama nchini Kenya (NTSA) kuondoa agizo hilo wakisema kuwa itawagharimu mno kufunga vidhibiti mwendo hivyo vipya na kuondoa vile vilivyopendekezwa mwanzoni.

  Wawakilishi wa wamiliki wa matatu kutoka Nairobi,Nyeri,nakuru,meru,Embu na Muranga,Kirinyaga,Tharaka Nithi na Kitui ni miongoni mwa waliokutana katika hoteli moja mjini Embu kupinga agizo hilo.

  Wakiongozwa na Abraham Gichovi,Rufus Kariuki,Francis Manyeki na Wanja Karuku,walilalamika kuwa wawekezaji katika sekta ya matatu walibebeshwa mzigo mkubwa kwa kulazimishwa kufunga aina mpya za vidhibiti mwendo miaka kadhaa iliyopita.

  Aidha wamiliki hao wa matatu walilalama kuwa vidhibiti mwendo vya sasa vinauzwa kati ya S35000 hadi S40,000 ikilinganishwa na vile vya awali ambavyo viluzwa Sh25,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako