• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Yanga yapangiwa Waarabu wa misri Kombe la Shirikisho

  (GMT+08:00) 2019-10-10 09:12:09

  Wawakilishi pekee Tanzania Klabu ya Yanga itamenyana na Pyramids ya Misri katika mechi mbili za nyumbani na ugenini kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hiyo ni baada ya droo iliyopangwa jana mjini Cairo nchini Misri na wawakilishi hao wa Tanzania wakifanikiwa kuvuka hatua hiyo wataingia kwenye makundi. Ratiba hiyo inaonesha Yanga itaanza kukipiga nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Oktoba 27 na mchezo wa marudiano utachezwa Novemba 03 huko Misri. Yanga imeangukia katika mchujo baada ya kutolewa na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia sare ya 1-1 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-1 Ndola. Kwa upande wa klabu za Kenya, Bandari FC itamenyana na Horoya AC ya Guinea na Gor Mahia itavaana na DC Motema Pembe ya DR Congo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako