• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Mataifa azungumzia uhusiano wake na China

    (GMT+08:00) 2019-10-11 09:00:21

    Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Hivi karibuni mkurugenzi wa idara ya mambo ya Afrika ya kituo cha mali za urithi cha Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa Bw. Edmond Moukala, alipohojiwa na mwanahabari wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, ameeleza mambo yake yanayohusika na China.

    Bw. Edmond Moukala ni mkurugenzi wa idara ya mambo ya Afrika ya kituo cha mali za urithi cha Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO. Mwezi Juni mwaka huu, aliendesha kongamano la ushirikiano katika ujenzi wa uwezo wa kushughulikia mali za urithi kati ya UNESCO, China na Afrika kwa lugha za Kichina, Kiingereza na Kifaransa. Kwa nini ofisa huyu wa Umoja wa Mataifa kutoka bara la Afrika anaweza kuongea vizuri lugha ya Kichina? Sababu ni kuwa babu moja yake alitoka mkoa wa Macao wa China, na ana damu ya kichina. Aidha, historia ya nchi yake inamfanya avutiwe zaidi na China. anasema,

    "Nchi yetu Jamhuri ya Kongo (Brazzaville) ilikuwa nchi ya kwanza ya kijamaa barani Afrika. Mambo ya China yameanza kujulikana wakati nilipozaliwa. Katika hospitali za nchi yetu, kulikuwa na madaktari wengi wa China. Nilipokuwa mdogo, kila mara nilipokuwa mgonjwa, wazazi wangu wakinipeleka kwa madaktari Wachina, nilikuwa na uhakika kuwa nitapona haraka. Na baada ya kuhitimu elimu ya sekondari, nilikuwa na machaguo matatu, yaani kusomea hisabati nchini Ufaransa, kusomea uhandisi wa ujenzi nchini Russia, na kusomea kilimo cha umwagiliaji nchini China. Niliamua kwenda kusoma China!"

    Bw. Moukala kwa mara ya kwanza alifika nchini China mwaka 1987, na hali ya wakati huo ya mji wa Beijing ilimwachia kumbukumbu kubwa. anasema,

    "Baada ya kufika uwanja wa ndege wa Beijing, tulipotoka mlango wa uwanja huo, tuliona wachina wakiandika habari za ndege kwa kalamu, hakukuwa na skrini ya kidigitali. Barabarani kulikuwa na farasi na mabasi madogo. Wakati huo hakukuwa na barabara kuu, na kulikuwa na barabara moja ya mzunguko tu. Ilikuwa nyuma kimaendeleo ikilinganishwa na hali ya hivi sasa mjini Beijing. Lakini jambo moja nina uhakika kuwa, wachina wa wakati huo walikuwa na nia thabiti, na walikuwa na fahari kubwa kuhusu utamaduni na mila zao. Nilikuja kusoma, lakini pia nilitaka kujua mambo mengine ya China, ikiwemo kwamba kwa nini wachina wanaonekana hivyo?"

    Nchini China kwa nyakati tofauti Bw. Moukala alijifunza lugha ya Kichina na elimu ya umwagiliaji. Wakati China ilipojenga Bwawa la Magenge Matatu, UNESCO ilitoa msaada mkubwa katika uhifadhi wa mabaki ya utamaduni. Bw. Moukala alipata ajira kwenye shirika hilo la kimataifa, na kufanya kazi katika ofisi ya UNESCO mjini Beijing kwa miaka 11. Hivi sasa anafanya kazi katika makao makuu ya shirika hilo mjini Paris, Ufaransa. Anafuatilia sana mambo ya China, na kushangaa kasi kubwa ya maendeleo ya nchi hiyo. Anasema,

    "Miaka 30 iliyopita, hakukuwa na mtu yeyote anayeweza kubashiri China itakuwa namna gani. Sasa nashangaa maendeleo makubwa yaliyopatikana nchini China, na nina imani kuwa China itakuwa na mustakabali mzuri zaidi katika siku za baadaye."

    Mabadiliko makubwa ya China yalimfanya Bw. Moukala awaze na kuwazua ni kwa nini China imepata maendeleo makubwa? Anaona kuwa sababu muhimu ni kuwa China imeshikilia historia na utamaduni wake wakati inapojiendeleza, na huu pia ni uzoefu wenye thamani kubwa unaostahili kuigwa na nchi za Afrika. Anasema,

    "Kama hatukubali na kutilia maanani utamaduni wetu, hatutapata maendeleo, kwani tutakosa nguvu ya ndani. Hili ni somo la kwanza nililopata nchini China. Hivyo niliposoma China, nilikuwa na uhakika kuwa, labda China haitaendelea leo au kesho, lakini iko siku itaendelea. Pia maendeleo yake yatabainika na yale ya Marekani au nchi za Ulaya. Kama aliyekuwa kiongozi wa China Hayati Deng Xiaoping alivyosema, aliiga uzoefu wa nchi za Ulaya na wa nchi nyingine, lakini ni lazima kuiendeleza China kwanza, halafu kuyakamilisha maendeleo hayo kwa kuiga uzoefu wa maendeleo ya nchi nyingine. Kama hujui unatoka wapi, wewe ni nani, na unakwenda wapi, na kama unatumia ovyo uzoefu wa watu wengine, basi utajiharibu mwenyewe."

    Alipoulizwa kuhusu maendeleo ya China katika siku za baadaye, alitaja pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Anaona kuwa pendekezo hilo si kama tu litahakikisha maendeleo ya China, bali pia litanufaisha utulivu na maendeleo ya nchi nyingine duniani, na hali hii inalingana na malengo ya Umoja wa Mataifa. Anasema,

    "Ikiwa mmoja wa wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China ni nchi pekee inayotekeleza mradi wa kimataifa ambao si kama tu inajinufaisha, bali pia inanufaisha nchi nyingine duniani. Hatukubali mtu yeyote kubaki nyuma kimaendeleo, Umoja wa Mataifa ulisema hivyo, na rais Xi Jinping wa China pia alisema hivyo. Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' ni mradi uliotupia macho mbali, na kutoa matumaini makubwa kwa watu wengi. Pia umetuletea soma jipya, kwamba tunategemeana. Aidha, pendekezo hilo limeleta matumaini kwa dunia na jumuiya ya kimataifa, na sisi sote tunajitahidi kuijenga dunia iwe nzuri zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako