• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eliud Kipchoge aongea kuhusu jaribio lake la kihistoria la Vienna

    (GMT+08:00) 2019-10-11 09:24:05

    Zikiwa zimesalia chini ya saa 24 kabla ya mwanariadha wa Kenya anayeshikilia rekodi ya mbio za marathon duniani Eliud Kipchoge kutimua vumbi na kutaka kuwa binadamu wa kwanza kukimbia umbali wa kilomita 42 chini ya muda wa saa mbili katika mbio za INEOS saa 1:59 Challenge, mwanariadha huyo amezungumzia kuhusu mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, Oktoba 12 mjini Vienna nchini Austria. Kipchoge alisema anafurahia sana kuwa mwanariadha wa kwanza kujaribu kukimbia kilomita 42 kwa muda usiozidi saa mbili. Aidha, Kipchoge ana matumani kuwa ataibuka mshindi wa mbio hizo na anajihisi kama Neil Armstrong alipozuru mwezini kwa mara ya kwanza mwaka 1969.

    "Kukimbia Berlin na kukimbia Vienna ni vitu viwili tofauti, kukimbia Berlin ni kuvunja rekodi ya dunia, na kukimbia Vienna ni kuweka historia, ni kujihisi kama binadamu wa kwanza kusafiri mwezini,"

    Muda rasmi wa kuanza mbio hizo utatangazwa leo Ijumaa, lakini utakuwa kati ya saa 12 asubuhi na saa nne asubuhi. Akijibu swali la mwanahabari baada ya kuulizwa atapata kiasi gani kama atavunja rikodi ya chini ya saa mbili anasema.

    "Nakimbia ili kuweka historia. Nakimbia ili kubadilisha kizazi. Nakimbia ili kuwaambia watu kuwa hakuna binadamu mwenye ukomo. Sikimbii kwa ajili ya pesa".

    Kipchoge, mwenye miaka 34, alitupa kete yake kwa mara ya kwanza kujaribu katika mbio za Monza Nike Breaking2 huko Monza, Italia Mei 6, 2017 ambapo alizidi kwa sekunde 26, na kutumia muda wa saa 2 na sekunde 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako