• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Taasisi, mashirika binafsi waaswa

    (GMT+08:00) 2019-10-11 19:01:49

    Taasisi, mashirika binafsi za asasi za kiraia, zimetakiwa kushirikiana na serikali ili kujenga jamii bora na taifa lenye maendeleo. Wakizungumza katika mkutano uliofanyika jana katika mkoa wa Arusha, kwenye kikao ambacho kiliwaleta pamoja wakurugenzi wa taasisi hizo, walisema kuna haja ya kujenga ushirikiano na mshikamano ili kujenga taifa imara na la kiuchumi. Ili kufanikisha haya, walidokeza kwamba lazima wajenge uhusiano mzuri na serikali ili kuwahudumia wananchi.

    Vile vile, swala la taasisi hizi kuwa na agenda ambazo zitawawezesha kuwa na sauti moja wakati wa kufanya mazungumzo na serikali kwa mstakabali wa taifa la Tanzania, lilijadiliwa.

    Ilibainikam kuwa awali, kulikuwepo na mashirika na taasisi ambazo zilikuwa na matumizi mabaya ya rasilimali na kutokuwa na uratibu mzuri wa shughuli zinazofanyika kwenye jamii. Kuhusu swala la serikali kuyaweka mashirika yote kwenye wizara moja, ni njia ya kuweza kuyafuatilia na kufanya tathmini ya utendaji kazi wao. Hii ni kutokana na baadhi ya mashirika hayo kukosa kuwa waaminifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako