• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya ngazi ya juu ya biashara kati ya China na Marekani yamalizika mjini Washington

    (GMT+08:00) 2019-10-12 18:30:25

    Naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni kiongozi wa China kwenye mazungumzo ya kiuchumi kati ya China na Marekani Liu He, mjumbe wa biashara wa Marekani Robert Lighthizer, na waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin walifanya mazungumzo ya raundi mpya kuhusu uchumi na biashara kuanzia tarehe 10 hadi 11 mwezi huu huko Washington.

    Kwenye mazungumzo hayo pande hizo mbili zilipata maendeleo kwenye kilimo, kulinda hakimiliki za ujuzi, kiwango cha ubadilishaji wa fedha, huduma za fedha, kupanua ushirikiano wa biashara, uhamishaji wa ufundi stadi na utatuzi wa migongano.

    Habari nyingine zimesema, rais Donald Trump wa Marekani jana alikutana na naibu waziri mkuu wa China Liu He na kusema anafurahia kuona mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya Marekani na China yanapata maendeleo. Vilevile amezitaka pande hizo mbili zithibitishe mapema waraka wa makubaliano ya mazungumzo ya kipindi cha kwanza, na kuhimiza zaidi mazungumzo ya baadaye. Pia amerejea tena kusema kuwa Marekani inakaribisha wanafunzi wa China kusoma nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako