• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • LANGALANGA: Valtteri Botas ashinda Japanese GP

  (GMT+08:00) 2019-10-14 08:43:34

  Valtteri Bottas jana alichupa kutoka watatu hadi wa kwanza na kuchukua taji la Japanese Grand Prix mbele ya Sebastian Vettel wa Ferrari na dereva mwenzake wa Mercedes, Lewis Hamilton. Charles Leclerc amemaliza wa sita hata hivyo mwisho amekuwa wa saba baada ya kupigwa penalti, na kwa vile sasa Bottas ameweza kumpita Hamilton kwenye msimamo, ina maanisha Mercedes inapata ushindi wa sita mfululizo. Baada ya ushindi huo, Bottas aliyemaliza ukame wa miezi sita wa kusubiri ushindi wake wa tatu wa 2019 baada ya kushinda katika mbio za magari mwanzoni mwa msimu nchini Australia na Azerbaijan mwezi April, alisema ingawa alianza wa tatu lakini kwa upande wake anaona alianza vizuri, kwani ameweza kuongoza na kuwa wa kwanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako