• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Mkenya Brigid Kosgei avunja rikodi ya dunia ya marathon

    (GMT+08:00) 2019-10-14 08:45:03

    Brigid Kosgei jana alivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Paula Radcliffe katika riadha za dunia za mbio za marathon kwa sekunde 8 na kutwaa ushindi katika kivumbi cha Chicago Marathon. Ushindi huo umeshuhudia ukifuta rikodi ya Radcliffe kutoka Uingereza aliyokuwa akishikilia kwa miaka 16 baada ya kukimbia kwa saa 2:15:25 April 13, 2003 huko London, na sasa amepokonywa na Kosgei ambaye aliandikisha muda wa saa 2:14:04. Kosgei alibainisha wazi kuwa angevunja rekodi ya Radcliffe, huku hali ya hewa jijini Chicago asubuhi, ikiwa shwari kwake kuandika jina lake katika vitabu vya kihistoria. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 alianza mbio hiyo kwa kuonyesha matumaini, kwa kukamilisha zaidi ya yadi tano kwa muda wa dakika 25:10 katika kasi ya historia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako