• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Nigeria yaikamata ndipo Brazil kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa na kushuhudiwa sare ya 1-1

    (GMT+08:00) 2019-10-14 08:45:26

    Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar jana alitoka kiwanjani akichechemea baada ya dakika 12 tu huku Brazil wakikamatwa ndipo na Nigeria kwenye mechi ya kirafiki na kushuhudiwa sare ya 1-1. Neymar alitoka kiwanjani akishikilia paja la kushoto na kutia wasiwasi kama ataweza kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya klabu ya Bruges Oktoba 22. Joe Aribo wa Rangers aliipatia Nigeria goli la uongozi kwenye nusu ya kwanza. Naye Casemiro wa Real Madrid alisawazisha bao la Nigeria dakika za mwanzo baada ya kuanza kipindi cha pili. Baada ya mechi Kocha wa Brazil Tite alisema Neymar alikuwa na maumivu ya misuli na alipumzishwa kama tahadhari. Licha ya kumiliki mpira kwa 70% nchini Singapore, Brazil hawakuweza kuondoka kifua mbele na kuendelea kutopata ushindi kwenye mechi hizi za kirafiki za kimataifa baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Senegal Alhamis wiki iliyopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako