• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa waraka kuhusu usalama wa chakula

  (GMT+08:00) 2019-10-14 17:37:54

  Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China leo imetoa waraka kuhusu usalama wa chakula. Waraka huo umeeleza mafanikio ya kihistoria iliyopata China katika kuleta usalama wa chakula, kuangalia kwa kina mfululizo wa sera na hatua za China katika kulinda usalama wa chakula baada ya mwaka 1996, haswa kufanyika kwa mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, kufafanua kanuni na msimamo wa China katika kufungua mlango na kufanya ushirikiano wa kimataifa kuhusu soko la chakula pamoja na utetezi wa sera wa China katika suala la chakula kwa siku za baadaye.

  Waraka huo umesema katika miaka 70 iliyopita, kutokana na uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China na juhudi kubwa, China ambayo msingi wa kilimo ulikuwa dhaifu sana na watu wake waliishi katika maisha magumu, imejitegemea na kufanikiwa kujitosheleza kwa chakula. SI kama tu imefanikiwa kutatua suala la chakula kwa watu wake bilioni 1.4, bali pia viwango vya maisha na lishe ya watu wake vimeinuka kidhahiri, na kwamba mafanikio makubwa ya kihistoria yamepatikana katika usalama wa chakula.

  Waraka huo umesema baada ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa 18 wa Chama, Kamati Kuu ya Chama inayoongozwa na rais Xi Jinping imelichukulia usalama wa chakula kama kipaumbele cha utawala wa nchi na kutoa mtazamo mpya wa usalama wa "kuhakikisha kujitosheleza kwa nafaka na chakula vinakuwa salama asilimia mia moja", na kuamua mkakati wa usalama chakula wa kutoa kipaumbele kwa soko la ndani la chakula, kuhakikisha uwezo wa uzalishaji, kuagiza chakula kutoka nje kwa kiasi kinachofaa na kutegemea uwezo wa teknolojia, ili kufuata njia ya usalama wa chakula chenye umaalum wa kichina.

  Waraka huo umesema China inashikilia sera ya kujitegemea kimsingi kwa chakula kinachozalishwa ndani ya nchi, kutekeleza kanuni kali ya kulinda maeneo ya kilimo, kutekeleza mkakati wa kupanga ipasavyo ardhi kwa ajili ya kilimo na kutegemea teknolojia katika kilimo", kuendelea kuhimiza mageuzi na uvumbuzi katika sekta ya kilimo, kuinua uwezo wa uzalishaji wa chakula, kukuza uchumi wa kilimo, kujenga mfumo wa ulinzi wa usalama wa chakula wa ngazi ya juu zaidi, ubora zaidi, ufanisi zaidi na endelevu zaidi, kuwa na nguvu zaidi katika kulinda usalama wa chakula, na kufuata kwa madhubuti njia ya usalama wa chakula wenye umaalum wa kichina.

  Waraka huo umesema China na Dunia zinategemeana kwa hatma zao katika kulinda usalama wa chakula, na China itaendelea kufuata kanuni za uwazi na ujumuishi, usawa na kusaidiana na ushirikiano na kunufaishana, kufanya juhudi kujenga muundo mpya wa kufungua mlango kwenye sekta a kilimo, kushirikiana na nchi mbalimbali duniani katika kulinda usalama wa chakula duniani na kutoa mchango mpya kwa ajili ya ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

  Wakati huohuo, Waraka huo umesema soko la chakula la China linazidi kufunguliwa kwa nchi za nje, na kwamba kiasi cha chakula kinachosindikwa na makampuni ya kigeni na mapato yake vinazidi kuongezeka, na mwaka jana kilichukua asilimia 14.5 na asilimia 17 ya jumla ya taifa la China mtawalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako