• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TUZO: Kipchoge, Cheruiyot wateuliwa kwenye tuzo za IAAF

    (GMT+08:00) 2019-10-15 08:46:51

    Mwanariadha anayeshikilia rikodi ya marathon duniani Eliud Kipchoge na bingwa wa mbio za mita 1500 Timothy Cheruiyot wameorodheshwa miongoni mwa wanariadha 11 walioteuliwa kwenye tuzo ya Mwanariadha Bora Duniani wa Kiume na Shirikisho la Riadha Duniani, IAAF, ambazo zitatolewa Novemba 23 huko Monaco, Ufaransa. Uteuzi wa Kipchoge unakuja siku mbili tu baada ya kuvunja rekodi ya kukamilisha mbio za marathon chini ya saa mbili katika kivumbi cha INEOS 1:59 Challenge jijini Vienna, Austria. Kipchoge, aliyeshinda tuzo za mwaka jana baada ya kuweka rikodi ya dunia huko Berlin, amekuwa kivutio zaidi na kutarajiwa kunyakua tuzo hiyo baada ya juzi kuandika historia ya "hakuna binadamu mwenye ukomo maalumu". Mbali na hapo pia alishinda Marathon ya London mwezi April ambapo aliweka rikodi ya saa 2:02:37. Kwa upande mwingine Cheruiyot naye ameshinda mbio za mita 1500 na kuondoka na dhahabu katika mbio za Doha, Qatar zilizomalizika hivi karibuni. Wawili hao watakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanariadha watatu Donavan Brazier, Christian Coleman na Noah Lyles.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako