• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ronaldo afikisha goli lake la 700

  (GMT+08:00) 2019-10-15 08:54:11

  Timu ya taifa ya Ureno usiku wa Oktoba 14 2019 walikuwa Ukraine kucheza mchezo wao wa kuwania kufuzu fainali za Euro 2020 dhidi ya Ukraine, mchezo ambao wengi walikuwa wakisubiria kwa hamu kumuona nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo akifikisha goli lake la 700 katika maisha yake ya soka. Goli la penati la Cristiano Ronaldo aliloifungia Ureno dakika ya 72 dhidi ya Ukraine iliyochapwa 2-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu Euro 2020, linamfanya Ronaldo atimize jumla ya magoli 700 katika maisha yake ya soka ambapo Sporting magoli 5, Man United magoli 118, Real Madrid magoli 450, Juventus magoli 32 na Ureno akifunga magoli 95. Goli la Ronaldo linamaanisha kuwa amejiunga na kundi la wachezaji wenye uwezo mkubwa kufikisha magoli 700 katika maisha yao ya soka. Kulingana na takwimu mshambuliaji huyo wa Juventus bado yuko nyuma sana ya mchezaji wa muda wote aliyefunga mabao mengi, Josef Bican aliyepachika jumla ya magoli 805. Mwingine ni Mbrazil Romario mwenye jumla ya magoli 772, huku mwenzake Pele akiwa watatu kwa magoli 767. Mchezaji wa Hungary Ferenc Puskas amefikisha magoli 746, na mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani Gerd Muller anakamilisha orodha ya wachezaji watano kwa kuwa na magoli 735.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako