• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira ya kiikolojia ya Mto Huanghe

    (GMT+08:00) 2019-10-15 16:48:26

    Jarida la Qiushi la China kesho litatoa makala muhimu ya rais Xi Jinping wa China ya "Hotuba kwenye semina kuhusu uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia ya Mto Huanghe na maendeleo yenye sifa nzuri".

    Kwenye makala hiyo, rais Xi amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira ya kiikolojia katika sehemu ambazo Mto Huanghe unapita. Ameagiza kushikilia wazo kwamba mazingira mazuri ya kiikolojia ni rasilimali, na kuweka kipaumbele katika uhifadhi wa mazingira na maendeleo yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira. Pia kutunga mipango ya maendeleo kwa kuzingatia uhifadhi wa maji ya Mto Huanghe, na kubainisha hali tofauti za sehemu tofauti, ili kuhakikisha usalama na utulivu wa muda mrefu wa mto huo, kuhimiza maendeleo yenye sifa nzuri ya uchumi, kuboresha maisha ya watu, kuhifadhi na kurithi utamaduni wa Mto Huanghe, na kuufanya mto huo kuwanufaisha zaidi watu.

    Makala hiyo imesema Mto Huanghe ni sehemu muhimu ya uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia na maendeleo ya uchumi, na pia ni sehemu muhimu ya kupambana na umaskini, na ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi na jamii na usalama wa mazingira ya kiikolojia nchini China, hivyo kuhifadhi mto huo ni mpango wa muda mrefu unaohusu ustawishaji wa taifa la China. Kama maendeleo sambamba ya Beijing, Tianjin na Hebei, maendeleo ya sehemu ya kiuchumi ya Mto Changjiang, na ujenzi wa ghuba kubwa ya Guangdong, Hong Kong na Macao, uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia na maendeleo yenye sifa nzuri ya Mto Huanghe pia ni mkakati muhimu wa kitaifa.

    Makala hiyo imesema, baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, mafanikio makubwa yamefiikiwa katika kushughulikia Mto Huanghe. Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, katika sehemu ya mtiririko wa Mto Huanghe, maendeleo makubwa ya uchumi na jamii yamepatikana, na maisha ya watu pia yameboreshwa kwa kiasi kikubwa, na pia, mazingira ya kiikolojia katika sehemu hiyo pia yameboreshwa. Hata hivyo, bado kuna changamoto mbalimbali, ikiwemo tishio la mafuriko, udhaifu wa mazingira ya kiikolojia, uchafuzi wa maji, na sifa ya maendeleo.

    Kwenye makala hiyo, rais Xi ameziagiza idara husika ziimarishe zaidi uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia katika Mto Huanghe, kuhakikisha usalama na utulivu wa muda mrefu wa mto huo, kutumia maliasili ya maji kwa ufanisi zaidi, kuhimiza maendeleo yenye sifa nzuri zaidi, na kuhifadhi, kurithi na kueneza utamaduni wa mto huo.

    Aidha, rais Xi ameagiza kufanya uvumbuzi katika kushughulikia mambo ya Mto Huanghe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako