• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Air Uganda yasaka mkurungezi

  (GMT+08:00) 2019-10-15 17:00:49

  Serikali ya Uganda inatafuta mkurungezi mkuu wa shirika la ndege nchini humo.

  Wizara ya uchukuzi iko kwenye mchakato wa kutafuta shirika litakaloendesha zoezi hilo kwanza kwa kuandaa tangazo la waliohitimu kutuma maombi.

  kwa sasa shirika hilo linaongozwa na Cornwell Muleya, lakini ni kaimu tu.

  Kabla ya kukaimu nafasi hiyo bwana Muleya alikuwa anahudumu kama mshauri wa kifundi kwenye shirika hilo.

  Katibu wa kudumu kwenye wizara ya uchukuzi bwana Waiswa Bageya amesema serikali inatafuta mkurungezi atakayesaidia shirika hilo kufanikiwa kibiashara ndani na je ya nchi.

  Wiki iliopita shirika hilo liliongeza ndege mbili mpya aina ya Bombardier ili kuliwezesha kuhudumu kwa miji zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako