• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa Afrika wana matarajio mazuri na Maonysho ya uagizaji ya China katika kupanua biashara

    (GMT+08:00) 2019-10-15 18:16:31

    Wakati maonyesho ya pili ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China (CIIE) yakikaribia kuanza mjini Shanghai, matarajio ni makubwa kuwa tukio hilo litaendelea kuchochea ukuaji wa biashara ya nje ya Afrika.

    Kampuni za Kenya, ambazo zilishiriki kwenye maonyesho hayo mwaka uliopita, zimekuwa ni mfano mzuri wa jinsi soko la matumizi la China linasaidia wauzaji wa Kenya kupanua biashara zao, na ni kwa nini wanataka kuendelea kutumia vizuri soko hilo ili kupata faida zaidi.

    Gazeti la Business Daily la nchini Kenya limenukuu takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Takwimu nchini humo mapema mwezi huu, kuwa China ilinunua bidhaa za Kenya zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 74 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 74 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho, hususan kutokana na usafirishaji wa mazao ya kilimo. Kahawa, chai maalum, maua na maparachichi ni baadhi ya mazao ya kilimo ambayo yanaendelea kupata soko kubwa nchini China.

    Ofisi ya Uchumi na Biashara ya Ubalozi wa China nchini Kenya hivi karibuni iliweka wazi kuwa, zaidi ya kampuni 12 za Kenya, ikiwemo zile za kilimo na chakula na pia za utalii, zitashiriki kwenye maonyesho ya pili ya Uagizaji wa Bidhaa Nje ya China.

    Kaimu katibu mkuu wa Shirikisho la Wafanyabiashara na Wanaviwanda nchini Kenya Bw. George Kiondo, ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, maonyesho hayo yanawasaidia wanachama wa Shirikisho hilo kufahamu fursa zinazopatikana nchini China. Amesema maonyesho hayo ni mazuri kwa ukuaji wa uchumi na jamii ya Kenya, na kuongeza kuwa hivi sasa, Kenya ni mwagizaji mkubwa na ili kukuza uzalishaji, maonyesho kama hayo yanahitajika ili kujitangaza zaidi. Bw. Kiondo amesema, kupitia maonysho hayo, Wakenya wanaweza kujifunza njia za uzalishaji hususan uzalishaji wa kuongeza thamani ya bidhaa na kujijengea uwezo ili waweze kuongeza usalishaji.

    Meneja mkuu wa kampuni ya Botanic Diamond nchini Kenya Cui Chaojie, anaiandaa kampuni yake kushiriki kwenye maonyesho hayo, na anataka kuleta bidhaa nyingi zaidi za Kiafrika katika soko la China. Anasema amekutana na mawakala wengi wa ununuzi katika Maonyesho ya kwanza ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China yaliyofanyika mwaka jana, na kutokana na fursa nyingi za manunuzi zilizopatikana kwenye maonyesho hayo, Cui amefungua duka huko Shenzhen na kujenga ghala la kuvuka mpaka mkoani Hong Kong mwaka jana.

    Wizara ya Biashara ya China imesema, takriban kampuni elfu tatu kutoka nchi na sehemu 150 zitashiriki kwenye maonyesho ya pili ya Uagizaji Bidhaa Nje ya China, ambayo yanatarajiwa kuanza Novemba 5 hadi 10 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako