• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maendeleo ya kasi ya miji na kukua kwa tabaka la kati barani Afrika vyavutia uwekezaji binafsi

    (GMT+08:00) 2019-10-16 08:15:57

    Ripoti mpya iliyotolewa jana mjini Nairobi inasema Afrika inashuhudia ongezeko la uwekezaji binafsi kutokana na maendeleo yanayoonekana kwenye bara hilo.

    Ripoti hiyo iliyotolewa na kampuni ya uwekezaji ya Cytonn yenye makao makuu yake mjini Nairobi, inataja kuwa maendeleo ya kasi ya miji, kupanuka kwa tabaka la kati na kuongezeka kwa matumizi vimechangia ukuaji wa uwekezaji binafsi barani Afrika.

    Ripoti inaongeza kuwa Eneo la Afrika Kusini mwa Sahara lina mustakbali mzuri zaidi wa kiuchumi ikilinganishwa na masoko mengine duniani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kenya, Nigeria na Ghana ni miongoni mwa nchi zinazovutia zaidi uwekezaji binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako