• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Jack Ma sasa kuangalia elimu, ujasiriamali na Afrika baada ya kustaafu

    (GMT+08:00) 2019-10-16 08:32:59

    Mwanzilishi wa kampuni ya Alibaba Bw. Jack Ma amesema kazi yake kubwa kwa sasa baada ya kustaafu ni kuangalia ni vipi elimu inaweza kutolewa kwa njia tofauti na kuwawezesha wajasiriamali vijana barani Afrika.

    Akiongea jana nchini Singapore Bw. Ma ambaye sasa ni mwenyekiti wa mfuko wa Jack Ma, amesema kwa sasa atatumia muda wake mwingi na nguvu zake kwenye elimu, hisani na ulinzi wa mazingira.

    Bw. Ma ambaye hapo awali alikuwa mwalimu, amesema elimu ya sasa bado inaendelea na mitizamo ya zamani inayosisitiza kupokea ujuzi darasani, lakini hali halisi ni kuwa watoto wengi wanapata ujuzi wao kupitia internet, na mashine na akili bandia zinaweza kufanya kazi nzuri zaidi kuchakata taarifa, kukumbuka na kukokotoa haraka zaidi kuliko binadamu.

    Amesema ili kuendana na mazingira ya sasa ya akili bandia, kazi inatakiwa kufanyika kubadilisha aina ya elimu inayotolewa na maudhui yanayofundishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako