• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WFP yasema mtu mmoja kati ya watu tisa duniani anasumbuliwa na njaa Kali

    (GMT+08:00) 2019-10-16 08:33:29

    Wakati leo dunia inaadhimisha siku ya chakula duniani, ripoti za kimataifa zinaonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, idadi ya watu wanaosumbuliwa na njaa duniani imeanza kuongezeka hadi kufikia watu milioni 882.

    Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema mmoja kati ya watu tisa duniani anasumbuliwa na njaa kali. Msemaji wa shirika hilo Bw Herve Verhoosel amesema wengi kati ya wanaosumbuliwa na njaa kali wako kwenye nchi zenye vita.

    Wakati hali ikiwa hivyo duniani, baadhi ya mataifa barani Afrika yapo kwenye hali mbaya ya ukosefu wa chakula ingawa shirika la chakula duniani FAO, linaitaja Tanzania kama moja ya mataifa yaliyofanikiwa kuwa na chakula cha kutosha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako