• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya milioni 13 ya wapiga kura watarajiwa kwenye siku ya uchaguzi mkuu nchini Msumbiji

    (GMT+08:00) 2019-10-16 08:49:06

    Tume ya taifa ya uchaguzi ya Msumbiji imesema, mchakato wa upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu umeanza kwa utulivu, na wagombea urais wamewataka wapiga kura wote washiriki kwenye mchakato wa kidemokrasia kwa utaratibu.

    Upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika jana ulishirikisha wagombea wanne wa urais, na vyama 26 vinagombea nafasi za wabunge na magavana wa majimbo. Hii ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kufanya uchaguzi mkuu usioshirikisha wagombea wa upinzani wa kihistoria, pia ni mara ya kwanza kuchagua magavana wa majimbo.

    Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi ya Msumbiji, watu takriban milioni 13.1 kati ya wamsumbiji milioni 30 walitarajiwa kupiga kura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako