• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • IMF yapunguza makadirio ya ongezeko la uchumi kwa mwaka huu

  (GMT+08:00) 2019-10-16 08:49:32

  Shirika la fedha duniani IMF limetoa Ripoti ya Makadirio kuhusu Uchumi wa Dunia, likipunguza makadirio ya ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka 2019 hadi asilimia 3, ambayo imepunguzwa kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na makadirio yaliyotolewa mwezi Julai. Hiki pia ni kiwango cha chini zaidi tangu msukosuko wa fedha ulipuke mwaka 2008.

  Ripoti hiyo imesema, kuongezeka kwa vizuizi vya kibiashara, kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na utulivu wa biashara na siasa za kijiografia, shinikizo la uchumi katika baadhi ya masoko yanayoibuka na makundi ya uchumi yanayoendelea, na masuala ya kimuundo ya makundi ya uchumi yaliyoendelea, vimesababisha kushuka kwa ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako