• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rais wa Chama cha Soka cha Bulgaria Borislav Mihailov ajiuzulu

    (GMT+08:00) 2019-10-16 09:12:13

    Rais wa Chama cha Soka cha Bulgaria Borislav Mihailov, amejiuzulu baada ya Waziri Mkuu wa Bulgaria Boyko Borissov jana kumtaka aache kazi kufuatia wachezaji wa England kufanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi na mashabiki wa nchi hiyo huko Sofia. Mchezo wa kufuzu kombe la Ulaya 2020, ambao umeshuhudia Uingereza ikiibamiza Bulgaria mabao 6-0, ulisimamishwa mara mbili kwasababu ya vitendo vya kibaguzi, vikiwemo kutoa saluti za Kinazi na kulia kama kima. BFU imesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na taharuki iliyozuka hivi karibuni lakini kwenye taarifa yake haikutaja vitendo ya kibaguzi. Serikali ya Uingereza imesema wataiandikia Uefa ili kutaka hatua zaidi zichukuiwe. Wakati huohuo rais wa Uefa Aleksander Ceferin amesema familia ya soka na serikali wanapaswa kuendeleza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi kwani mashirikisho ya soka hayawezi kutatua suala hili peke yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako