• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Rwanda yatoa wito wa ushirikiano katika kukabiliana na majanga wakati wa msimu wa mvua

  (GMT+08:00) 2019-10-16 18:40:12

  Waziri wa Usimamizi wa Mambo ya Dharura nchini Rwanda Germaine Kamayirese ametoa wito wa ushirikiano zaidi ili kukabiliana na majanga ya kimaumbile wakati wa msimu wa mvua.

  Akizungumza mjini Kigali, Bi. Kamayirese amesema wadau wote wakiwemo viongozi na wananchi kwa ujumla wanapaswa kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji wa kina wa hatua za kupunguza majanga. Amewataka raia wanaoishi kwenye maeneo yaliyo hatarini zaidi kuhamia maeneo salama, na kuitaka jamii kuboresha mifumo ya mitaro ya kupitisha maji, kujenga kingo na kufuata maelekezo sahihi ya ujenzi wa nyumba ili kupunguza athari za majanga ya kimaumbile.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako