• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Jumuiya ya waliosoma China wazindua Sacco

    (GMT+08:00) 2019-10-16 19:48:45
    Katika mkutano wa siku moja wa kimkakati uliofanyika Dar es Salaam ukilenga kuwakutanisha waliosoma China ili kujadili fursa zilizopo kati ya nchi hizo mbili,Jumuiya ya watanzania waliosoma China (CAAT),wamezindua chama cha kuweka akiba na mikopo (Sacco)

    Akizungumza katika mkutano,Mgeni rasmi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddm,aliipongeza CAAT kwa kuandaa mkutano huo.

    Alisema sera za Tanzania kwa sasa zimelenga kuinua uchumi wa nchi.

    Alisema ni wakati mzuri kwa wanajumuiya hao kutumia Sacco hiyo kuanzisha biashara na viwanda kutokana na uwepo wa mazao yatokanayo na kilimo,uvuvi,ufugaji, na rasilimali zilizopo.

    Makamu Mwenyekiti wa Sacco hiyo ya CAAT,Dk Fatma-Roselyn Waziri,alisema kupitia sacco hiyo,hisa zitanunuliwa na wataweka akiba na kukopesha wanajumuiya kama njia moja ya kuinua wanajumuiya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako