• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya-Rais Kenyatta azindua awamu ya 2A ya SGR Nairobi-Naivasha

  (GMT+08:00) 2019-10-16 19:52:25

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo jumatano alizindua rasmi awamu ya 2A ya reli ya kisasa (SGR) kutoka Nairobi hadi Naivasha pamoja na kuanzisha ujenzi wa barabara kuu kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) hadi eneo la Westlands.

  Shughuli kuu ya uzinduzi ilifanyika katika kituo cha SGR cha katika eneo la Mai Mahiu.

  Aidha huduma ya treni ya kubeba abiria itaanza rasmi kesho alhamisi huku ile ya uchukuzi wa mizigo ikianza baada ya miezi kadhaa ijayo.

  Huduma hiyo ya uchukuzi wa abiria itapatikana tu katika vituo vinne kati ya 12 katika awamu hiyo ya SGR.

  Vituo hivyo ni pamoja na Ongata Rongai, Ngong, Mai Mahiu na Suswa.

  Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, kampuni ya China Communication and Construction Company iliyojenga reli hiyo imekuwa ikiendesha safari za majaribio kama sehemu ya maandalizi kwa uzinduzi wa leo Jumatano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako