• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RUGBY: Shujaa yaanza michuano ya Safari Sevens ikivaana na Zambia

    (GMT+08:00) 2019-10-17 08:37:41

    Timu ya Taifa ya Kenya ya rugby kwa wachezaji saba, Shujaa inatarajiwa kuanza kampeni yake ya Safari Sevens dhidi ya Zambia mchezo ambao utachezwa Jumamosi saa 5 asubuhi baada ya kutoka sare na timu hiyo ya Kusini mwa Afrika katika kundi C. Shujaa, wanaowania kurejesha taji lao ambalo mara ya mwisho walishinda mwaka 2016, pia watacheza na klabu ya Blue Bulls ya Afrika Kusini na Russia Academy katika mechi za utangulizi kwenye mashindano ya siku tatu, yatakayoanza kuchezwa kesho kwenye uwanja wa RFUEA. Wakati Shujaa ikijitafutia njia ya kufika robo fainali, timu ya Morans ya Kenya itakabiliwa na kibarua kigumu baada ya kupangwa kundi A pamoja na mabingwa wa Dunia mwaka 2017/18 Afrika Kusini ambao wametaja timu bora yenye wafungaji wenye pointi za juu Cecil Afrika. Uganda, washiriki wa kila siku kwenye Safari Sevens tangu yaanzishwe mwaka 1996, wapo kundi moja na Burundi. Nao mabingwa watetezi Samurai Select, walioitoa Shujaa na kuwa mabingwa wa michuano iliyopita wapo kundi B, ambalo pia lina timu ya Western Province kutoka Afrika Kusini, Klabu ya Russian Narvskaya Zastava na Red Wailers ya Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako