• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua ujenzi wa barabara ya kasi iliyojengwa kwa fedha za China mjini Nairobi

    (GMT+08:00) 2019-10-17 08:50:47

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amezindua ujenzi wa mradi wa barabara inayojengwa kwa fedha kutoka China ambayo itasaidia kupunguza msongamano katika mji wa Nairobi.

    Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 26.8 ni barabara ya kwanza ya namna hiyo nchini Kenya, na inatarajiwa kusaidia kuboresha miundo mbinu ya Kenya. Rais Kenyatta amesema baada ya barabara hiyo kukamilika Kenya itakuwa na barabara kama za nchi zilizoendelea.

    Mradi huo utatekelezwa kwa pamoja kati ya mamlaka ya taifa ya barabara kuu ya Kenya na kampuni ya ujenzi wa barabara na madaraja ya China.

    Mamlaka hiyo imesema mradi huo utagharimu dola milioni 599 na utakamilika ndani ya miaka mitatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako