• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la utawala nchini Sudan latangaza kusimamishwa vita nchi nzima

    (GMT+08:00) 2019-10-17 08:51:14

    Mwenyekiti wa baraza la utawala nchini Sudan Bw. Abdel Fattah Al-Burhan ametoa amri ya kikatiba ya kusimamisha mapambano katika nchi nzima.

    Amri hiyo inasema uamuzi wa kusimamisha vita umetolewa ili kuweka mazingira ya kufanikisha amani na usalama katika nchi nzima. Amri hiyo imetolewa baada ya kundi la SPLM tawi la Kaskazini linaloongozwa na Abdelaziz al-Hilu kutangaza kusimamisha mazungumzo na serikali ya Sudan, hadi matakwa yake yote yatakaposhughulikiwa, ikiwa ni pamoja na kuachiwa huru kwa wanachama wake waliokamatwa.

    Mazungumzo kuhusu kutafuta amani ya Sudan yanafanyika mjini Juba nchini Sudan Kusini, kati ya serikali ya Sudan na makundi yenye silaha kutoka Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako