• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Tanzania amfukuza kazi ofisa wa kupambana na ufisadi kwa kutokuwapo mkutanoni

  (GMT+08:00) 2019-10-17 08:56:18

  Rais John Magufuli wa Tanzania ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi ya siku nne kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara, amemfukuza kazi ofisa mwandamizi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Mtwara, kutokana na kutokwepo kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji cha Chigugu, wilayani Masasi.

  Rais Magufuli alimwita ofisa huyu kwenye mkutano huo uliotangazwa moja kwa moja na TBC, na kumtaka afafanue namna ya ofisi yake ilivyoshughulikia hasara ya mamilioni ya Shilingi ambazo ziliripotiwa kutengwa kwa ajili ya kuwalipa wakulima wa karanga.

  Baada ya kuambiwa kuwa hayupo kwenye msafara wa rais, rais Magufuli amemwagiza kaimu mkurugenzi wa TAUKURU Bw. Johan Mbungo amkabidhi ofisa huyo majukumu mengine, na kumteua ofisa mwingine kuchukua nafasi yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako