• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia yatafuta kupanua soko la kahawa kwenye CIIE

  (GMT+08:00) 2019-10-17 09:02:37

  Ethiopia inatafuta kupanua uuzaji wa kahawa isiyo na kemikali na kukuza soko lake kwenye maonyesho ya pili ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China CIIE.

  Ofisa Masoko katika mamlaka ya kahawa na chai Ethiopia Bw. Tatek Girma, amesema kahawa ni moja ya bidhaa zinazopewa kipaumbele na Ethiopia kuuzwa nchini China. Mamlaka hiyo inashirikiana na wafanyabiashara na mashirika husika kwa ajili ya kushiriki vizuri kwenye maonyesho hayo yatakayofanyika mjini Shanghai.

  Mkurugenzi mkuu wa shirikisho la uuzaji wa kahawa nchini Ethiopia Bw. Gizat Worku, amesema maonyesho hayo ni fursa nzuri ya kukuza uuzaji wa kahawa isiyo na kemikali ya Ethiopia katika soko la China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako