• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNHCR laahidi kuisaidia Afrika Kusini kuongeza ufanisi wa mfumo wa hifadhi ya wakimbizi

  (GMT+08:00) 2019-10-17 09:10:40

  Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeahidi kuisaidia Afrika Kusini kuzidisha ufanisi wa mfumo wa hifadhi ya wakimbizi na kuboresha upatikanaji wa nyaraka kwa wakimbizi na watafutaji wa hifadhi.

  Shirika hilo limesema limetambua kuwa kama nchi nyingine nyingi, Afrika Kusini inakabiliwa na changamoto inayoletwa na mzunguko wa watu unaoongezeka siku hadi siku.

  Afisa mwandamizi wa shirika hilo nchini Afrika Kusini anayeshughulikia mambo ya mawasiliano Bw. Helene Caux, amesema mifumo ya hifadhi ya wakimbizi imekumbwa na shinikizo kubwa kutokana na mapigano na mateso kuwafanya wakimbizi wengi zaidi kuvuka mipaka, wakati upatikanaji wa hifadhi wa wakimbizi ukikabiliwa na ukosefu wa machaguo ya uhamiaji wa kawaida na salama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako